BAN KI MOON AMUAGA DL. ASHA-ROSE MIGIRO
Friday, June 29, 2012
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Mkewe, anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na Mumewe, Profesa Cleophas Migiro wakisubiri kusalimiana na wageni waalikwa wakati wa hafla ambayo Ban Ki Moon aliandaa maalum kwajili ya kumuaga msaidizi wake wa Karibu.
Waalikwa wakijichanganya ukumbini wakati wa sherehe hiyo
Profesa Migiro akiwa na Bint yake, Chansa- Jasmin wakifuatilia hafla hiyo kwa makini
� t n a �/� �� :p>
Ban Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo amempogeza na kushukurusu sana Migiro kwa namna alivyokuwa mshauri wake na mwalimu wake ambaye a anasema kwa ualimu wake anampa alama ya plus plus plus. akatumia hafla hiyo kutangaza kwamba anamteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika. Migiro anaondoka baada ya kuutumikia Umoja wa Mataifa kwa miaka mitano na nusu.
Na Chiaziiiiiiiiiiiiiiiii iligongeshwa, Katibu Mkuu akitakiana kila la kheri na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. -Asha Rose Migiro, kulia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Bw. Anyanga.
Bi Amina Mtengeti akinywa kinywaji chake baada ya kigongeshana chiaziiiiii na Katibu Mkuu Ban Ki Moon
Dk. Migiro akibadilishana mawazo na Dk. Ki-Moon
Hata kupiga picha naweza. Naibu Katibu Mkuu akinyaka tukio hili la picha wakati Katibu Mkuu Ban Ki Moon akizungumza na Bint wa mwisho wa Migiro Chansa Jasmin
COPA COCACOLA CUP YAZIDI KUPAMBA MOTO
Thursday, June 28, 2012
Mshambuliaji wa timu ya Vijana ya Kilimanjaro, Ridhiwani Yussuf (kulia) akimtoka beki wa Shinyanga Frank Zololo, timu zao zilipomenyana leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, katika mfululizo wa michuano ya Timu ya Vijana ya Copa Cocacola. Pichani ni 'move' ya Ridhiwani na Zololo hatua kwa hatua
1
2
3
DK.ULIMBOKA ALIPOFIKISHWA MUHIMBILI BAADA YA KUPIGWA NA KUUMIZWA VIBAYA NA WATEKA NYARA
Ilikuwa pilipika pilika ya aina yake.
Ni wakati Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanbzania, Dk. Steven Ulimboka alipofikishwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuokoa maisha yake, yaliyokuwa yanachungulia kifo, baada ya kupigwa hadi kujeruhiwa vibaya ya watu wasiojulikana ambao walimteka nyara na kumpeleka hadi msitu wa Mabwepande ambako walimpiga na inasemekana amevinjwa baadhi ya viongo, kungolewa kucha na meno.
Moja ya yaliyojitokeza ni ushirikiano wa ajabu wa madaktari uliojitokeza, tangu kumsubiri hadi kuwasili kwake hospitali ya Muhimbili Dk. Ulimboka akiwa mahututi.
Madaktari hao ambao wapo katika mgombo licha ya kuzuiwa na mahakama, walionekana kusitisha mgomo wao kwa wakati huo na kuingia 'kazini' kumhudumia Ulimboka.
Wakati wakimhudumia Ulimboka, madaktari kwa madaktari , wagonjwa wengine walikuwa hawapati huduma kufuatia mgomo kuwepo kwa wagonjwa.
Inaelezwa baada ya kuingizwa wodi ya Taasisi ya Mifupa (MOI) kwenye hospitali hiyo ya Muhimbili, zaidi ya madaktari 20 walizunguka kumtibu D. Ulimboka.
Ilikuwa mpambano wa hali ya juu hasa kati ya wapigapoicha na maofisa usalama na polisi, huku hali ikiwa ya kutisha pale watu wanaosaidikiwa ni madaktari walipoamua kumshambulia Ofisa wa Polisi aliyekuwa kazini miomngoni mwa polisi waliokuwepo kujaribu kudhibiti aina yoyote ya rabsha ambayo inesababishwa na mapokezi ya majeruhi, Dk. Ulimboka.
Hatma ya mgomo huo hadi sasa haijajulikana, ingawa leo Waziri Mkuu alitarajiwa kutoa uamuzi wa serikali kuhusu madaktari waliomi katika mgomo huo, lakini leo hii hakuweza kufanya hivyo kutokana na angalizo la kadhia hiyo kuwepo mahakama kuu.
Tayari hadi sasa Mahakama kuu imeshazuia mgomo huo, lakini madaktari nao kupitia Jumuia yao wameendelea kukaidi.

Subscribe to:
Comments (Atom)