Ni wakati Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanbzania, Dk. Steven Ulimboka alipofikishwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuokoa maisha yake, yaliyokuwa yanachungulia kifo, baada ya kupigwa hadi kujeruhiwa vibaya ya watu wasiojulikana ambao walimteka nyara na kumpeleka hadi msitu wa Mabwepande ambako walimpiga na inasemekana amevinjwa baadhi ya viongo, kungolewa kucha na meno.
Moja ya yaliyojitokeza ni ushirikiano wa ajabu wa madaktari uliojitokeza, tangu kumsubiri hadi kuwasili kwake hospitali ya Muhimbili Dk. Ulimboka akiwa mahututi.
Madaktari hao ambao wapo katika mgombo licha ya kuzuiwa na mahakama, walionekana kusitisha mgomo wao kwa wakati huo na kuingia 'kazini' kumhudumia Ulimboka.
Wakati wakimhudumia Ulimboka, madaktari kwa madaktari , wagonjwa wengine walikuwa hawapati huduma kufuatia mgomo kuwepo kwa wagonjwa.
Inaelezwa baada ya kuingizwa wodi ya Taasisi ya Mifupa (MOI) kwenye hospitali hiyo ya Muhimbili, zaidi ya madaktari 20 walizunguka kumtibu D. Ulimboka.
Ilikuwa mpambano wa hali ya juu hasa kati ya wapigapoicha na maofisa usalama na polisi, huku hali ikiwa ya kutisha pale watu wanaosaidikiwa ni madaktari walipoamua kumshambulia Ofisa wa Polisi aliyekuwa kazini miomngoni mwa polisi waliokuwepo kujaribu kudhibiti aina yoyote ya rabsha ambayo inesababishwa na mapokezi ya majeruhi, Dk. Ulimboka.
Hatma ya mgomo huo hadi sasa haijajulikana, ingawa leo Waziri Mkuu alitarajiwa kutoa uamuzi wa serikali kuhusu madaktari waliomi katika mgomo huo, lakini leo hii hakuweza kufanya hivyo kutokana na angalizo la kadhia hiyo kuwepo mahakama kuu.
Tayari hadi sasa Mahakama kuu imeshazuia mgomo huo, lakini madaktari nao kupitia Jumuia yao wameendelea kukaidi.
0 comments:
Post a Comment