Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Mkewe, anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na Mumewe, Profesa Cleophas Migiro wakisubiri kusalimiana na wageni waalikwa wakati wa hafla ambayo Ban Ki Moon aliandaa maalum kwajili ya kumuaga msaidizi wake wa Karibu.
Waalikwa wakijichanganya ukumbini wakati wa sherehe hiyo
Profesa Migiro akiwa na Bint yake, Chansa- Jasmin wakifuatilia hafla hiyo kwa makini
� t n a �/� �� :p>
Ban Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo amempogeza na kushukurusu sana Migiro kwa namna alivyokuwa mshauri wake na mwalimu wake ambaye a anasema kwa ualimu wake anampa alama ya plus plus plus. akatumia hafla hiyo kutangaza kwamba anamteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika. Migiro anaondoka baada ya kuutumikia Umoja wa Mataifa kwa miaka mitano na nusu.
Na Chiaziiiiiiiiiiiiiiiii iligongeshwa, Katibu Mkuu akitakiana kila la kheri na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. -Asha Rose Migiro, kulia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Bw. Anyanga.
Bi Amina Mtengeti akinywa kinywaji chake baada ya kigongeshana chiaziiiiii na Katibu Mkuu Ban Ki Moon
Dk. Migiro akibadilishana mawazo na Dk. Ki-Moon
Hata kupiga picha naweza. Naibu Katibu Mkuu akinyaka tukio hili la picha wakati Katibu Mkuu Ban Ki Moon akizungumza na Bint wa mwisho wa Migiro Chansa Jasmin
0 comments:
Post a Comment